Atimiza ndoto ya kuoa wake wawili kwa siku moja - EDUSPORTSTZ

Latest

Atimiza ndoto ya kuoa wake wawili kwa siku moja

 


Kiongozi wa chama cha vijana All Progressives Congress (APC) Mjini Abuja nchini Nigeria, Babangida Sadiq amefunga ndoa na wake zake wawili kwa siku moja huku akidai ametimiza ndoto zake ambazo alikuwa anatamani kufanya hivyo tangu alivyokuwa mtoto.

 


Harusi zake zote zimefanyika siku ya Jumamosi Machi 6 mjini Abuja, na wake zake wamefahamika kwa majina ya Maryam Muhammad na Maimuna Mahmud, harusi ya kwanza imefanyika saa 4 Asubuhi nyingine imefanyika 7 Mchana.


Akizungumzia sababu ya kuoa wake wawili baada ya kufunga ndoa Babangida Sadiq amesema "Kwa muda mrefu ndoto zangu ilikuwa kuoa wanawake wawili kwa siku moja, watu wengi wanahisi haiwezekani lakini Mungu amefanya nimefanikisha hili" No comments:

Post a Comment