AS Vita, TP Mazembe Wamlilia Rais Magufuli-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

AS Vita, TP Mazembe Wamlilia Rais Magufuli-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

BAADA ya kusikia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania John Magufuli, kiungo wa kati wa Klabu ya AS Vita, Jeremy Mumbere amemlilia rais huyo huku akisema kuwa yeye alikuwa ni kati ya shabiki mkubwa wa kiongozi huyo. Jeremy Mumbere kwa sasa ni nahodha wa kikosi cha AS Vita na timu ya Taifa ya DR Congo.

 

 

Akizungumza na Championi Ijumaa moja kwa moja kutoka nchini DR Congo, Mumbere alisema kuwa amesikitishwa kusikia taarifa za kifo cha Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kwani alikuwa ni kiongozi mzuri ambaye alikuwa akimfuatilia kwa ukaribu kutokana na utendaji wake kuwa mzuri jambo ambalo lilimfanya awe anamfuatilia mara kwa mara.

 

 

“Nimesikitika sana kusikia taarifa za msiba wa Rais wa Tanzania, John Magufuli ni moja kati ya rais bora kuwahi kutokea katika bara hili la Afrika, alikuwa ni kiongozi anayependa maendeleo na Tanzania ilikuwa imepata mengi mazuri kutoka kwake.

 

 

“Utendaji wake wa kazi ulinifanya niwe shabiki yake kwa kumfuatilia kwa mambo mengi, hakika Tanzania imempoteza mtu wa muhimu sana kwani hata huku DRC tulikuwa tunampenda sana Rais Magufuli,” alisema kiungo huyo.

 

 

Naye mwenyekiti wa mashabiki wa Klabu ya TP Mazembe, Jean Mazembe Kazadi alisema: “Niwape pole Watanzania wote na Afrika kwa jumla kwa kumpoteza Rais Magufuli, nasema Afrika kwa jumla kwa kuwa ndiye alikuwa kioo kwa viongozi wengi hapa Afrika katika maamuzi ambayo wengi walikuwa hawezi kasoro yeye ambaye alikuwa akithubutu, wote tumuombee Magufuli,” alisema kiongozi huyo.

The post AS Vita, TP Mazembe Wamlilia Rais Magufuli appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz