-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MSAFARA wa watu 38 ukiwa na wachezaji 24 wa Yanga na viongozi 14 wa timu hiyo, leo Alhamisi utasafiri ku-wafuata Mbeya City kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa wikiendi hii.

 

Katika msafara huo, kiungo mshambuliaji raia wa Burundi, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ ameachwa jijini Dar akipewa program maalum kutokana na kutokuwa fiti ambapo hivi sasa anafanya mazoezi ya gym.Timu hizo zinatarajiwa kuvaana keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili.

Akizungumza na Spoti Xtra, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa, alisema kuwa maandalizi kuelekea mchezo huo yamekamilika na kikubwa wanakwenda Mbeya kufuata pointi tatu lengo likiwa ni kuendelea kukaa kileleni katika msimamo wa ligi.

Mfikirwa alisema timu hiyo inatarajiwa kusafiri leo alfajiri kwa ndege ambapo wameamua kutumia usafiri huo ili kutowachosha wachezaji kutokana na umbali wa safari hiyo.

“Maandalizi ya mchezo yamekamilika na msafara wetu utakuwa wa watu 38, kati ya yao wachezaji 24 na viongozi 14 watakaosafiri na timu,” alisema Mfikirwa huku akiwataja wachezaji watakaosafiri ni;Metacha Mnata, Farouk Shikalo, Mukoko Tonombe, Lamine Moro, Tuisila Kisinda, Bakari Mwamnyeto, Waziri Junior, Zawadi Mauya, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Deus Kaseke na Farid Mussa.Wengine ni Said Makapu, Adeyum Saleh, Paul Godfrey ‘Boxer’, Omari Chibada, Dickson Job, Ditram Nchimbi, Yacouba Songne, Fiston Abdoul Razack, Haruna Niyonzima, Michael Sarpong, Feisal Salum na Carlos Carlinhos.

The post Yanga Yaifuata Mbeya City Full Mziki appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand