-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MABINGWA wa kihistoria Tanzania, Yanga wamesema kuwa hawajapokea taarifa rasmi za kufungiwa kufanya usajili na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).

 

Hiyo ikiwa ni siku moja tangu zianze kuzagaa taarifa za FIFA kuifungia Yanga kufanya usajili kufuatia sakata la madai kutoka kwa aliyekuwa mshambuliaji wa Amisi Tambwe.

 

FIFA ilitangaza kuifungia Yanga kwa kile kilichotajwa kutomlipa mshambuliaji huyo madai yake ya Sh milioni 44 yaliyotokana na usajili wake.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela, alisema kuwa bado hawajapokea rasmi barua kutoka FIFA, lakini kama ikifika basi hawana tatizo watazilipa fedha hizo.

 

Mwakalebela alisema kuwa mashabiki wasiwe na hofu juu ya hukumu hiyo ya FIFA, wamejipanga vema kufanikisha hilo na wataendelea kufanya usajili kama kawaida.

 

“Tumeona hizo taarifa katika mitandao ya kijamii, lakini nataka niwatoe hofu Wanayanga kuwa hilo halipo mezani kwetu na kama lipo kulipa hizo fedha siyo tatizo kwetu.

 

“Mashabiki wa Yanga wasiwe na wasiwasi kabisa hizo milioni 44 tutazilipa haraka iwezekanavyo, tulivyoingia madarakani tulikuta madeni mengi katika timu, hivi sasa tumeyalipa na tunaendelea kuyalipa,” alisema Mwakalebela.

 

Alipotafutwa Tambwe kuzungumzia hilo, alisema: “Hiyo adhabu waliyoitoa FIFA ni kweli, lakini kama watalizilipa hizo fedha wataruhusiwa kuendelea na usajili kama kawaida.

The post Yanga Yaahidi Kumlipa Tambwe appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand