-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

IMEELEZWA kuwa Klabu ya Yanga imefungiwa na FIFA kufanya usajili wa miaka mitatu kutokana na madai ya kutomlipa fedha za usajili pamoja na mshahara mchezaji wao wa zamani Amiss Tambwe.

 

Kawaida FIFA hutoa adhabu kama hiyo kwa timu zilizoshindwa kutimiza agizo lake na hasa suala la malipo.

Habari za uhakika kabisa kutoka Zurich nchini Uswisi zinaeleza kuwa Yanga ilipewa siku 45 kumlipa mshambuliaji wake wa zamani Amissi Tambwe fedha anazowadai na muda huo ulishapita bila kulipwa.

 

Yanga bado hawajalipa hata senti kwa Tambwe ambaye anadai dola 19,000 ambazo ni zaidi ya Sh milioni 43.7 na FIFA imewataka Yanga kuongeza asilimia 5 ikiwa kama ya usumbufu kwa mchezaji huyo.

Imeelezwa kuwa Tambwe anadai fedha hizo zikiwa za mishahara ya miezi miwili pamoja na kiasi kidogo ambacho hawakumlipa katika fedha yake ya Usajili.

The post Yanga Wafungiwa Na Fifa Kufanya Usajili Kisa Tambwe appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand