-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa hautendewi haki kwenye masuala yao tofauti na wengine namna ambavyo wanafanyiwa ikiwa ni pamoja na sakata la mchezaji wao Bernard Morrison ambaye kwa sasa anakipiga ndani ya Simba.

 

Morrison amekuwa na mvutano mkubwa na mabosi wake hao wa zamani ambapo wao wanadai kwamba ana kandarasi ya miaka miwili ndani ya Yanga huku mchezaji akiweka wazi kuwa alisaini dili la miezi sita.

 

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredric Mwakalebela mwishoni mwa 2020 aliweka wazi kuwa mchezaji huyo alisaini mkataba feki jambo ambalo limefumbiwa macho na wahusika pamoja.

 

Pia amesema kuwa Morrison alitakiwa kulipa fedha kwa kwa Yanga ila mpaka sasa imekuwa kimya tofauti na wao wanapofanya makosa kupewa adhabu mara moja.

 

Mwakalebela amesema:”Mkataba feki wa mchezaji mpaka sasa imekuwa kimya, tunaomba tuitwe tuthibitishe, ukweli kuhusu suala hilo ila tunamaliza ligi hatujaitwa.

 

“Kamati ilisema mchezaji anapaswa arudishe fedha kwenye Klabu ya Yanga, hadi leo hakuna suala hilo kuona linazungumzwa na hakuna majibu na hakuna suala linalozungumziwa.

 

“Hatujasskia TFF,(Shirikisho la Soka Tanzania) likisema kuwa mchezaji huyo amelipa ama kuna taarifa yoyote inayohusu malipo yake.

“Ila ikitokea sasa ni suala la Yanga limetokea muda huohuo adhabu inatolewa kwa wakati na utaskia tunaambiwa kwamba tunakatwa kwenye mapato ya getini,” .

The post Yanga Wadai Wanaonewa, Waibua Upya Sakata La Morrison -Video appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand