-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa nyota wao waliosajiliwa ndani ya kikosi hicho wakiongozwa na Fiston Abdulazak ambaye ni mshambuliaji pamoja na Said Ntibanzokiza ‘Saido’ watarejesha furaha ya timu hiyo ya kutwaa ubingwa.

 

Tayari nyota huyo ambaye ni raia wa Burundi ameanza mazoezi baada ya kujiunga rasmi kwa dili la miezi sita anakutana na mshikaji wake Saido ambaye kwa sasa anatibu majeraha yake aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh alisema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kuweza kutwaa ubingwa huku wachezaji waliosajiliwa wakiwa na kazi ya kurejesha furaha.

“Mashabiki wetu pamoja na uongozi kiujumla tunatambua kwa muda mrefu hatujatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, hivyo wachezaji wetu wote ikiwa ni pamoja na Fiston, Saido, Yacouba Sogne, Dickson Job wanaweza kutimiza malengo yetu.

 

“Tunacheza tukiwa ni timu kila mmoja anafanya kazi kwa ushirikiano hivyo mashabiki wazidi kutupa sapoti pale ligi itakaporejea tutakuwa imara,” alisema Hafidh.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA | CHAMPIONI

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

WAZIRI MKUU AWEKWA KIKAANGONI BUNGENI KWENYE KIKAO CHA TATU

The post Yanga: Subirini Muone Moto wa Fiston, Saido appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand