-->

Type something and hit enter

On


MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo Feburuari 4, 2021, imesema imetafakari uamuzi wake wa kuifungia kwa muda wa miezi sita Wasafi TV  baada ya kituo hiko kuwasilisha maombi na vielelezo zaidi ikiomba mamlaka kupitia upya uamuzi uliotolewa.

 

Taarifa ya TCRA imeeleza, Wasafi TV iliwasilisha ushahidi kuonyesha endapo ushahidi huo ungewasilishwa wakati wa usikilizwaji, mamlaka isingeweza kutoa adhabu hiyo. Pia, walikiri kurusha matangazo mubashara kinyume na masharti ya leseni.

 

Wasafi TV itatumikia adhabu hadi mwisho wa mwezi huu Februari 28, 2021, na imetakiwa kuzingatia masharti ya leseni. Ikishindwa au kukaidi uamuzi, TCRA imesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa.


Click to comment
 
Blog Meets Brand