-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KUELEKEA mechi za hatua ya makundi kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika, timu ya Al-Merreikh ya nchini Sudan imemtimua kocha wake Mserbia Miadrag Jesic ambaye alichukua nafasi ya Didier Gomes, aliyetimkia Simba.

 

Jesic alitambulishwa rasmi kwenye kikosi cha Al-Merreikh Januari 25 mwaka huu, lakini juzi Jumatatu klabu hiyo ilithibitisha kuachana na Mserbia huyo bila kutaja sababu yoyote ya kumvunjia mkataba akidumu kwenye kikosi hicho kwa takribani wiki moja.

 

Klabu hiyo ilimtangaza Mbelgiji Nesreddine Nabi kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho ambacho kipo kundi A, kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika na timu za Simba, AS Vita na Al Ahly.

 

Aidha klabu hiyo pia imeendelea kuimarisha kikosi chake baada ya kufanikiwa kuinasa saini ya mshambuliaji wa timu ya taifa ya Jamaica na nyota wa zamani wa Klabu ya DC United ya nchini Marekani Darren Dimitri Mattocks, ikiwa sehemu ya maboresho ya kikosi hicho kuelekea mechi za hatua ya makundi.

Stori: Hussein Msoleka, Dar es Salaam

The post Wapinzani wa Simba Waajiri Kocha Mpya appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand