KIKOSI cha Simba leo Februari 3, 2021 baada ya kutinga Makao Makuu ya nchi, Dodoma kimepata nafasi ya kuingia ndani ya Bunge la Tanzania wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Barbara Gonzalez na Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara .

Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Barbara Gonzalez akiongea jambo na Msemaji wa klabu, Haji Manara wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge la Tanzania muda huu ambapo kikao kinaendelea.
Miongoni mwa wachezaji waliopo bungeni ni pamoja na Gadiel Michael, Ibrahim Ajibu, Said Ndemla, Shomari Kapombe, Clatous Chama, Mohamed Hussein.
Kenedy Juma, Hassan Dilunga, Ibrahim Ame,Beno Kakolanya, Aishi Manula, Pascal Wawa,Mzamiru Yassini, Luis Miquissone.
Benchi la ufundi ni pamoja na Kocha Mkuu, Didier Gomes kocha msaidizi, Seleman Matola.
Mratibu wa Simba Abbas Seleman,Ofisa Habari wa Simba Haji Manara.

Picha ya pamoja ya wabunge, mtendaji mkuu wa klabu, wachezaji na benchi la ufundi wakiwa nje ya Bunge la Tanzania.
The post Wachezaji wa Simba na Benchi La Ufundi Watua Bungeni, Dodoma appeared first on Global Publishers.