-->

Type something and hit enter

On


LICHA ya kwamba ni mama mwenye mtoto mkubwa tu, Krish Ndikumana, staa wa Bongo Movies, Irene Uwoya, eti ametamba kwamba, bado ana muda mrefu wa kuendelea kula ujana wake vizuri bila kuwa na mwanaume yeyote wa kuishi naye ndani mpaka atakapoona ametosheka vilivyo ndipo atakapofikiria kuolewa.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, Uwoya au Mama Krish anasema kuwa, kuna wakati mwingine baadhi ya wanawake wanakuwa hawajamaliza kula ujana vizuri hivyo wakiingia kwenye ndoa hawakai na mwisho wa siku ndoa inavunjika.


“Wanawake wengi wanakimbilia kwenye ndoa mapema, lakini baada ya muda ndoa inavunjika maana bado wanatamani sana mambo ya nje na hata mimi nimejifunza hivyo kwa sasa nakula kwanza ujana mpaka nitosheke, halafu nikishaingia kwenye ndoa, nitakaa kwa kutulia,” anasema Uwoya mwenye umbo matata.

Stori: Khadija Bakari, Dar


Click to comment
 
Blog Meets Brand