UEFA: Manchester City Yaendeleza Balaa-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest

UEFA: Manchester City Yaendeleza Balaa-Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

Matajiri wa jiji la Manchester nchini England, klabu ya Manchester City imeendeleza mwendo wake wa ushindi na sasa kufikisha ushindi wa michezo 19 mfululizo kwenye michuano yote baada ya usiku wa jana kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Borrusia Moenchengladbach.

 

 

Ushindi huo unawafanya Manchester City kuwa na faida ya mabao mawili ya ugenini na kuwa na uwezekano mkubwa wa kutinga hatua inayofuata ya Robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Barani Ulaya kuelekea mchezo wake wa mkondo wa pili unaotaraji kuchezwa tarehe 16 Machi mwaka huu.

 

 

Mabao ya City yamefungwa na kiungo Bernardo Silva na mshambuliaji wake Gabriel Jesusu na kuweka rekodi ya kufunga kwenye michezo yake yote mitano ya hatua ya 16 bora ya michuano hiyo katika misimu yake minne akiwa na Manchester City.

 

 

Kwa upande mwingine, licha ya timu hiyo ya Wananchi wa jiji la Manchester ‘The Citizens’, kuutawala mchezo kwenye maeneo yote lakini kocha wa timu hiyo, Mhispania Pep Guardiola hakuonekana kuridhishwa na idadi hiyo ya mabao.

 

 

“Kiujumla, tuliutawala mchezo. Haikuwa bahati hatukuwa sahihi vyakutosha kuweza kuzitumia nafasi za mabao tulizozitengeneza. Hiki ni kitu ambacho tunapaswa kukiboresha kwenye michuano hii. Kwenye michuano hii inapswa uwe na usahihi wa hali ya juu ili uhakikishe unasonga mbele”.

 

 

Katika kujibia nafasi ya City kuwa bingwa wa michuano hiyo baada ya kuwa na mwendo mzuri, Pep amesema “Nilipoiona Bayern Munich jana sikuwezi kufikiria hivyo. Kwasasa naifikiria Westham United . Kama watu wanasema hivyo inabidi tukubali, sio tatizo, tunakubali”.

 

 

Mabingwa watetezi, Bayern Munich ilipata ushindi wa mabao 4-1 ugenini dhidi ya Lazio ya Italia usiku jana. Manchester City jumamosi ya kesho kutwa tarehe 27 Februari 2021, inatazamiwa kushuka dimbani kukipiga na ‘Wagonga nyundo wa jiji la London’ klabu ya Westham United kwenye ligi kuu nchini England.

 

 

Manchester City wakipata ushindi basi wataifikia rekodi ya kushinda michezo 20 mfululizo kwenye michuano yote kama walivyofanya mwaka 2017.

The post UEFA: Manchester City Yaendeleza Balaa appeared first on Global Publishers.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.