-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MSHAMBULIAJI mkongwe wa TP Mazembe na timu ya taifa ya DRC Congo, Tresor Mputu amefunguka kuwa Simba ina uwezo mkubwa wa kuifunga AS Vita pindi watakapokutana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Simba na AS Vita katika Ligi ya Mabingwa Afrika wamepangwa katika Kundi A huku wakitarajia kukutana katika mchezo wa kwanza ambao AS Vita watakuwa wenyeji utakaofanyika Februari 12 nchini Congo.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi,Mputu alisema kuwa kutokana na uwezo mkubwa ambao ameuona kutoka kwa Simba pindi walipokutana katika fainali ya Simba Super Cup anaamini unaweza kuwafanya kuwa washindi dhidi ya AS Vita.

 

“Simba hii ambayo tumecheza nayo ni tofauti na zote ambazo tuliwahi kucheza nazo huko nyuma, kwa sasa Simba ina wachezaji wengi wazuri wenye uwezo wa kuwapa matokeo hata katika michezo muhimu na migumu ndiyo maana naamini hata watakapokutana na AS Vita wakipambana vizuri wanaweza kupata ushindi.“

 

Hata katika ligi ya mabingwa wanaweza kufika mbali kutokana na aina ya wachezaji wazuri walionao hivyo wanatakiwa kuendelea kupambana zaidi hasa kuongeza uwezo wa kufunga zaidi mabao na si kumiliki tu mpira bila kufunga mabao naamini itawasaidia zaidi,” alisema mshambuliaji huyo.

Stori: Marco Mzumbe, Dar es Salaam

The post Tresor Mputu: Simba SC inaweza kuifunga AS Vita appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand