Siri Yaficuka, Sababu ya Billnas Kumwagana na Nandy - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Siri Yaficuka, Sababu ya Billnas Kumwagana na Nandy
WAKATI msanii wa Bongofleva, Faustina Charles ‘Nandy’ akithibitisha kuachana na mchumba wake ambaye pia ni msanii mwenzie William Lyimo ‘Billnass’, RISASI limenyaka sababu tatu zilizotajwa kuwa chanzo cha uchumba wao kuvunjika.

 

 

Wawili hao ambao ni mojawapo ya ‘couple’ maarufu iliyojizolea mashabiki wengi nchini, walidaiwa kuwa kwenye mipango ya ndoa ikiwa ni miezi michache baada ya Billnass kumvisha Nandy pete ya uchumba.

 

 

Hata hivyo, katika mahojiano yaliyofanyika juzi na kituo kimoja cha redio, Nandy alisema, “Siko tayari kulizungumzia sana kwa undani ila utofauti upo na haya ni mambo ya kawaida katika mahusiano. Tuna muda mrefu… We are not ok, ila sio kitu kikuubwa tumepeana break kidogo. Ni vitu vya kawaida.”

 

 

Nandy na Billnass wamedumu kwenye uhusiano kwa muda wa miaka minne lakini ukiwa ni uhusiano uliotafsiriwa kuwa wa ‘in and out’ SABABU HIZI HAPA KOFFI ATAJWA Tangu mkongwe wa muziki wa rhumba, Koffi Olomide atue nchini Januari 26 mwaka huu, kumeibuka fununu za Nandy na mchumba wake kutemana.

 

 

Fununu hizo zilizidi kuota mizizi baada ya Billnass kutohudhuria shoo ya Koffi na Nandy katika ukumbi wa Mlimani city hali iliyoibua maswali mengi bila majibu.

 

 

Hata hivyo, ujio wa Koffi ambaye ameshirikishwa na Nandy wimbo wa Leo leo, ulidaiwa kumuweka Nandy bize na mkongwe huyo huku Billnass akionekana kuwa mnyonge katika baadhi ya party alizohudhuria kipindi hicho.

 

 

NDUGU NAO WAPO

Suala la Billnass kukataliwa ukweni lilidaiwa kuibuka siku nyingi na kusababisha fununu kuwa ndugu wa Nandy hawamtaki staa huyo wa Hip hop. Ukweli huo ulikaribia kudhibitishwa na Dada yake Nandy, aliyejitambulisha kwa jina la Salma pindi alipokuwa akizungumza na chanel moja ya mtandaoni.

 

 

Julai 25 mwaka jana, Dada Nandy aliweka wazi kuwa bado ni mapema sana kwa mdogo wake kuolewa. “Bado kwa mimi na familia yetu, tunaona kuwa Nandy muda wa kuolewa bado, hata mimi nilikaa uchumba miaka mingi, mpaka ninakuja kuolewa… kwa sababu ndoa ya kikristo hamuachani labda mkimbilie mahakamani. Kwa hiyo mtu anatakiwa kukaa na kufkiria ili msikurupuke,” alisema.

 

 

Kauli hiyo ya Dada yake Nandy ilikuja miezi michache baada ya Billnass kumvisha pete Nandy. Billnass alimvisha pete Nandy Aprili 10 mwaka jana katika hafla ambayo ilihudhuriwa na ndugu wachache.

 

 

UMAARUFU WATAJWA

Aidha, wachambuzi wa masuala ya kisaikolojia na kimahusiano, walisema umaarufu wa Nandy ambao ni dhahiri amemzidi Billnass vilevile unaweza kuwa chanzo cha wawili hao kuachana.

 

 

Mmoja wa watalaam hao, Mseco Kidee alisema dalili za kuyumba kwa mahusiano ya ambayo mwanamke anaonekana kuwa nguvu aidha ya kiuchumi, au umeaarufu kuliko mwenzie huonekana dhahiri. Alisema hali hiyo inaweza kujitokeza iwapo wawili hao hawatokuwa wamejenga mahusiano yao katika misingi imara.

 

 

Alitolea mfano uchumba wa Nandy na Billnass ambao ulionekana kulegalega tangu awali na kuongeza kuwa ni jambo ambalo halikuwashtua wengi ingawa mashabiki walitamani wawili hao wadumu pamoja.

 

 

WALIKOTOKA NI MBALI

Wawili hao ambao waliwahi kufunguka kuwa kwa mara ya kwanza waliandika ukurasa wa kimapenzi katika tour ya tamasha maarufu la Fiesta lililofanyika mkoani Mbeya mwaka 2016, wamepitia milima na mabonde mengi hali iliyotarajiwa na wengi kuwa sasa walipaswa kufunga ndoa.

 

 

Kwa mfano suala la kukataliwa ukweni, Billnass aliwahi kukanusha na kudai kuwa ni maneno ya mtandaoni. “Kuhusu kukataliwa ukweni, sidhani kama ni kweli, lakini pia wakwe zangu mimi ni watu wa dini sana, hivyo nisingependa kuwaongelea sana kwenye media yoyote ile kwa sababu ninachokijua mimi ni kwamba, wananipenda kama mtoto wao na wamenikubali,” alisema Billnass alipozungumza na gazeti hili mwaka jana.
Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click πŸ‘‰πŸ‘‰πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz