-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

 

MAKAMU mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salim Muhene ‘Try Again’ alisema katika uongozi wa klabu hiyo umekuwa na ushirikiano mzuri na taasisi na vyombo vinavyohusika na soka hapa nchini, huku wakisema wametenga bilioni 6.

 

 

Akizungumza jana kabla ya uchaguzi mdogo wa Simba wa kuziba nafasi ya mwenyekiti, Try Again alisema suala la mchakato wa mabadiliko ndani ya klabu hiyo linatarajiwa kumalizika mapema mwaka huu.

 

 

“Hatuna matatizo na Tume ya Taifa ya Ushindani (FCC), kwa upande wetu, Simba haijkosea ilikwenda FCC kwa ajili ya kutafuta msaada na kila kitu kinakwenda vizuri na mchakato huo unaenda kukamilika,” alisema Try Again.

 

 

Alisema ndani ya uongozi wao kuna mambo mengi ya kufanya kuhakikisha wanafikia malengo yanayotarajiwa na Wanasimba pamoja na timu hiyo kucheza mpira na kuhakikisha wanaenda kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya nne mfululizo.

 

 

Kwa upande wa mapato na matumizi ya mwaka 2019/20, afisa mkuu wa fedha, Yussuf Nassoro, aliweka wazi kwamba mwaka huu jumla ya mapato yalikuwa Billion 6 katika fedha hizo bill.2.6 zilitolewa Mo Dewji.

 

 

“Kwa matarajio ya mwaka 2020/21 ili kutimiza mambo yanayotakiwa na Simba, mapato yatakuwa bill. 5.4 na matumizi yetu bill.6.5, hivyo tuna upungufu ya bill. 1, Bodi inaendelea kufanyia kazi kuhakikisha inapata ongezeko la fedha hizo,” alisema afisa mkuu huyo wa fedha.

 

 

Naye Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez, alipopewa nafasi alisema anapambana kuhakikisha anafanikiwa kutimiza vigezo alivyopewa na bodi hiyo ikiwemo kutetea ubingwa wa ligi pamoja na FA, kufikia makundi ambayo wapo na sasa kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa pamoja na Simba Queens kutetea ubingwa.

 

 

“Tumefanya vizuri katika usajili wetu kuongeza wachezaji kwa timu zote mbili huku tukifanya maboresho timu yetu ya wanawake kwa kumpa ulezi Fatma Dewji,” alisema Barbara.

 

 

Hii inaonyesha kuwa fedha hizo bilioni 6 ndiyo zitaisaidia Simba kutwaa ubingwa bara, timu ya wanawake kutetea ubingwa wake pamoja na kufika nusu fainali ya Klabu Bingwa Afrika kama walivyopanga.

 

Issa Liponda na Wilbert Molandi, Dar es Salaam.

The post  Simba Yatenga Bilioni Sita Za Ubingwa appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand