-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KILICHOBAKIA ni kusubiri dakika 90 zitoe majibu mara baada ya kikosi cha Simba kuwa tayari kusaka ushindi wa kwanza dhidi ya AS Vita huku viongozi wakiwa wameshamaliza kila kitu nje ya uwanja.

 

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara amesema wamepambana na kila aina ya dalili ya hujuma na fitna ambazo zilikuwa zinainyemelea timu hiyo ndiyo maana hadi sasa hakuna taarifa ya majeruhi wala Covid-19 kwa wachezaji na benchi la ufundi.

Simba itashuka hii leo Ijumaa saa 4 usiku kutupa karata yake ya kwanza ugenini kwenye mchezo wa Kundi A utaochezwa kwenye Uwanja Stade De Martyrs, Kinshasa nchini DRC Congo, huku wakiwa na kumbukumbu ya kuchapwa 5-0 kwenye uwanja huohuo msimu wa 2018-19.

“Tumekuja kusaka heshima ya nchi na klabu kwa jumla. Sisi kama viongozi tumejitahidi kupambana kwa kila namna kuona hakuna baya lolote linatokea kwa wapambanaji wetu,” alisema Manara.

STORI: ISSA LIPONDA, Dar es Salaam

The post Simba Kila Kitu Fresh DR Congo, Wapangua Fitna Zote appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand