-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

ZIKIWA zimebaki siku nne pekee kabla ya kuwavaa Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, presha imeshuka ndani ya kikosi cha Yanga baada ya wachezaji watatu kati ya wanne waliokuwa majeruhi kuanza rasmi mazoezi ya pamoja na wenzao.

 

Nyota walioanza mazoezi na wenzao kujiandaa na mchezo wa Mbeya City ni beki Dickson Job na washambuliaji, Yacouba Songne na Michael Sarpong huku kiungo mshambuliaji Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ akiwekwa chini ya uangalizi wa madaktari wa klabu hiyo.Saido anasumbuliwa na matatizo ya misuli ambayo aliyapata kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons.

 

Akizungumza na Championi Jumatano,Meneja wa kikosi cha Yanga, Hafidh Saleh alisema kikosi hiko kinaendelea na maandalizi ya mwisho tayari kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Mbeya City.

 

“Kikosi chetu kinaendelea na maandalizi ya mwisho ya mchezo dhidi ya Mbeya City, tunashukuru kuwa kati ya wachezaji wanne waliokuwa na majeraha watatu tayari wameanza mazoezi ya pamoja na wenzake.

 

“Sarpong, Yacouba na Job wote wako vizuri aliyebaki ni Saido ambaye bado yuko chini ya uangalizi wa madaktari wanaoangalia maendeleo yake,” alisema Saleh.

Yanga ndiyo vinara wa msimamo wa ligi na pointi zao 44 walizokusanya katika michezo 18 waliyocheza mpaka sasa wakishinda mechi 13 na kutoa sare kwenye michezo mitano.

 

Saido amekuwa mkombozi kwenye kikosi Yanga baada kufanikiwa kufunga mabao mawili ya ligi na kutoa pasi tatu zilizozaa mabao.

LIVE​​: MAGAZETI FEB 10 – NI FUNGA KAZI, NAPE ACHARUKIA UKUSANYAJI KODI…

The post Saido Awekwa Chini ya Ulinzi… appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand