RAIS wa miamba ya soka Real Madrid ya nchini Hispania, Fiorentino Perez jana mchana Februari 2 amekutwa na maambukizi ya Covid-19 na kuchukua tahadhari ya kujiweka karantini ili maambukizi hayo yasienee kwa watu wengine klabuni hapo.
Perez anakuwa mtu wa kwanza kwenye mwezi Februari kuripotiwa kuwa na maambukizi hayo klabuni hapo baada ya mchezaji, Nacho Fernandes kupatwa na ugonjwa huo siku tano zilizopita na ataukosa mchezo wa La Liga dhidi ya Huesca Verona jumamosi ya wiki hii.
Wakati Perez anapata maambukizi hayo, kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amepimwa na kukutwa hana maambukizi hayo baada ya kupata matibabu na kukaa karantini kwa siku na mbili na kupelekea kukosa michezo miwili ya La Liga ukiwemo waliofungwa na Levante 2-1.
Baadhi ya waliougua ugonjwa huo klabuni hapo ni pamoja na, kocha wa Real Madrid ya vijana ‘Castilla’, Raul Gonzalez aliyeugua Januari 19 wakati mshambuliaji wa klabu hiyo Eden Hazard alipata maambukizi hayo mwezi Disemba
The post Rais wa Real Madrid, Perez Akutwa na Corona appeared first on Global Publishers.