-->

Type something and hit enter

OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB
TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes imeanza vibaya Fainali za Kombe la Mataifa kwa Vijana chini ya umri wa miaka 20, (AFCON U20) baada ya kuchapwa 4-0 na Ghana usiku wa jana Uwanja wa Manispaa ya Nouadhibou Jijini Nouadhibou nchini Mauritania.
Katika mchezo huo wa Kundi C, mabao ya Ghana yalifungwa na Percious Boah dakika ya tatu na 71, Abdul Fatawu Issahaku dakika ya 30 na Joselpho Barnes dakika ya 89 – wakati mechi nyingine ya kundi hilo jana, Morocco iliichapa Gambia 1-0, bao pekee la El Mehdi Moubarik dakika ya 26. 
Baada ya mchezo huo, kocha wa Ngorongoro Heroes, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ alisema ugeni wa mashindano ndiyo ulisababisha wafungwe 4-0 na Ghana.


Ngorongoro Heroes itashuka tena dimbani Februari 19 kumenyana na Gambia kabla ya kukamilisha mechi zake za Kundi hilo kwa kumenyana na Morocco Februari 22,hapo hapo Uwanja wa Manispaa ya Nouadhibou.


Click to comment
 
Blog Meets Brand