-->

Type something and hit enter

On 


Ni 'headlines' za African Princess Nandy ambaye ametusanua kuwa wimbo wake mpya aliofanya na msanii Koffi Olomide kutoka Congo DR, umemgharimu zaidi ya shilingi Milioni 70.

 

Akifunguka hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, Nandy amesema hana shaka yoyote kuhusu gharama za wimbo hata kama asipompa faida ila anachoamini ni kwamba atakuwa ameacha alama kwenye muziki wake.

 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE

"Sijaongeza sifuri mbele ila kwa mtu muelewa anajua ilivyo, kuna kurekodi video ambayo si chini ya Milioni 15 au 16,  kumvalisha Koffi Olomide na watu wake, wachezaji, mimi mwenyewe, magari na hoteli zenye hadhi ya nyota tano zaidi ya Milioni 70, hata kama faida ikichelewa naamini itakuwa imeniachia alama" amesema NandyClick to comment
 
Blog Meets Brand