-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KIKOSI cha Namungo FC kimerejea hotelini usiku wa kuamkia leo Februari 14 baada ya kushindwa kuondoka  jijini Luanda, Angola kurejea Tanzania ikitumia kutwa nzima ya jana ikiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Luanda.

Namungo imeshindwa kusafiri kwa ndege ya kukodi baada ya wachezaji wake watatu na kiongozi mmoja ambao inadaiwa  waliokutwa na maambukizi ya virusi vya #Corona kutoruhusiwa na mamlaka kutoka karantini kujiunga na wenzao kwa ajili ya safari hiyo.

Awali Shirikisho  la Soka Afrika (CAF) liliufuta mchezo huo wa Kombe la Shirikisho kati ya CD de Agosto ya Angola dhidi ya Namungo FC ya Tanzania uliopangwa kufanyika jana Februari 14.

 

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirikisho la Soka nchini (TFF), sababu za kufutwa mchezo huo ni taratibu za #COVID19 ambapo mamlaka za Angola ziliutaka msafara wa timu yote ya Namungo kuwekwa karantini mara baada ya kuwasili nchini humo.

 

The post Namungo Yashindwa Kurejea Tanzania appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand