-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

UONGOZI wa Klabu ya Namungo, umesema kuwa maamuzi ya Kamati Maalum ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kupanga michezo yote miwili ya hatua ya 32 bora kati ya timu hiyo dhidi ya Clube Desportivo 1ยบ de Agosto ya Angola ipigwe jijini Dar, ni faida kubwa kwao.

 

 

Hatua hiyo imekuja baada ya Namungo kurejea nchini waki­tokea Angola ambapo walikumbana na ma­tukio mengi yaliyofanya mchezo wao uliopangwa kuchezwa wikiendi iliyopita kuahirishwa na CAF.

 

 

Uamuzi huo wa Kamati Maa­lum ya CAF iliyokuwa ikishughu­likia sakata hilo, ume­kuja baada ya kubainika kuwa si wenyeji wa mchezo huo wa awali wala Namungo, iliyohusi­ka moja kwa moja kukwamisha mechi hiyo, hivyo kuamuru mechi zote mbili kuchezwa angalau ndani ya saa 72, na ziwe zi­mechezwa kufikia Februari 26.

 

 

Agosto watakuwa mwenyeji wa mechi ya kwanza, huku Namungo wao wakiwa wenyeji kwenye mchezo wa pili.

 

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Namungo, Kindamba Namlia, alisema: “Maamuzi yaliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika tumeyapokea, na hatuwezi kuyalalamikia kwa sababu wao wamefanya tathimini ya kile ambacho kilitokea Angola na kuja na maamuzi hayo.

 

 

“Jambo zuri ni kwamba wakati huu sisi tutakuwa nyumbani, kimazingira hii ni faida kwetu na kikosi tayari kimeanza mazoezi tangu Jumanne kuelekea mchezo wetu wa kwanza ambao tutacheza Februari 21, hatuna majeruhi yoyote.”

 JOEL THOMAS, Dar es Salaam

The post Namungo Yachekelea Waangola Kuletwa Dar appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand