-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KIUNGO mkabaji wa Yanga, raia wa DR Congo, Mukoko Tonombe amefichua kuwa amekuwa akipambana kwa kuhakikisha Yanga inapata ushindi katika kila mchezo kwa kuwa ana deni la kuipa ubingwa timu hiyo kutokana na sapoti kubwa wanayopewa na mashabiki wao.

 

Mukoko amejiunga na Yanga akitokea AS Vita ya DR Congo amefanikiwa kufunga bao moja kati ya 29 yaliyofungwa na vinara hao wakiwa na pointi 44 na leo watacheza na Mbeya City.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Mukoko alisema: “Jambo kubwa ni kwamba bado tupo juu, tunaongoza ligi hivyo tunachokiangalia kwa sasa nikuendelea kubakia pale kwa kujitoa katika kila mchezo ili tuweze kuendelea kupata matokeo mazuri kwa sababu malengo ni kuchukua ubingwa.

 

“Unajua nipo hapa kwa ajili ya mashabiki sasa lazima nijitoe kwa kusaidia timu kupata matokeo na kuona inapata ushindi maana kwangu naona hili deni ambalo natakiwa kulilipa kwa kuhakikisha timu inachukua ubingwa ili mashabiki wanaotupa sapoti wapate furaha kama ilivyokuwa kwenye Kombe la Mapinduzi.”

Stori: IBRAHIM MUSSA, Dar es Salaam

The post Mukoko: Nina Deni la Ubingwa Yanga SC appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand