-->

Type something and hit enter

By On



Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MASHABIKI wa soka jijini hapa wanazungumzia zaidi uwepo wa Bernard Morrison na Chris Mugalu kwenye kikosi cha Simba kitakachowavaa AS Vita Ijumaa saa 3 usiku.

 

Simba imetua Kinshasa na wachezaji 27 ili kujiweka tayari kwa lolote linaloweza kutokea hata kama baadhi yao watakumbana na mizengwe ya ugonjwa wowote.

 

Kwa mujibu wa mchambuzi na mtangazaji mahiri wa michezo kwenye redio maarufu ya Top Congo FM, Jenovic Mbowa wachezaji hao wawili ndio wanaosemwa sana na wanapewa nafasi kubwa ya kusumbua kwa vile wanaielewa vizuri DR Congo na aina ya soka na mambo ya ndani na nje ya uwanja.

 

Alisema Morrison kama akiongeza umakini kwenye kufunga ndiye anayeweza kuwa na madhara zaidi ndani katika mechi hiyo kwa vile wanamjua.

 

“Mugalu ni mchezaji mzuri na isitoshe ni Mkongo, anaelewa mambo mengi ya hapa kwa vile alicheza sana FC Lupopo ya Lubumbashi anawajua sana Vita, atasumbua,” alisema.

 

The post Morrison, Mugalu Gumzo Kila Kona DRC appeared first on Global Publishers.



Click to comment
 
Blog Meets Brand