-->

Type something and hit enter

On


MABINGWA watetezi wa Ligi kuu bara Simba, leo Februari 18 wamefanikiwa kuibuka na ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya Biashara United ya mkoani Mara, na kufanikiwa kuvuna pointi tatu muhimu.
 
Mchezo huo umechewezwa katika dimba la Karume Musoma, bao pekee la Simba limepachikwa wavuni na Bernard Morrison dakika ya 22 ya mchezo.
 

 
Simba ambayo haikuanza na baadhi ya nyota wake ilitengeneza nafasi kadhaa za wazi kufunga na kama Morrison na Chikwende wangetumia vema nafasi hizo, wekundu wa msimbazi Simba wangeshinda kwa zaidi ya goli moja.
 
Kwa matokeo hayo Simba imefikisha alama 42 baada ya kucheza michezo 18 katika nafasi ya pili, Yanga inaongoza msimamo kwa alama 46 baada ya kushuka dimbani mara 20.
 
Click to comment
 
Blog Meets Brand