-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa Didier Gomes amewapiga biti zito wapinzani wake AS Vita ya DR Congo kwa kusema wapo tayari kwa ajili ya kucheza nao.

 

Kocha huyo amebainisha kuwa wako tayari kwa ajili ya mechi hiyo kutokana na aina ya uimarikaji wa timu hiyo kwa killa siku.

 

Mfaransa huyo atawaongoza Simba katika mechi yao ya kwanza ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kucheza na AS Vita Februari 12, nchini Congo.Gomes ameliambia Championi Jumatatu, kuwa kwake hana hofu kuhusiana na mechi hiyo kutokana na kwamba kikosi chake kimekuwa kikibadilika kwenye mechi ambazo wamezicheza hadi sasa.

 

“Tunafahamu tutacheza na As Vita Februari 12 kule Congo lakini hatuna hofu sana na mechi hiyo kwa sababu timu imekuwa na maendeleo mazuri kila baada ya siku.

 

“Tumekuwa tukipambana kila kwenye mechi kufanya vizuri, hali ambayo inatufanya twende kwenye mechi hiyo tukiwa kamili.“Uzuri zaidi ni kwamba tumekuwa tunabadilika kutokana na mpinzani ambaye tunacheza nae,” alimaliza Mfaransa huyo na kuongeza:“

 

Kikosi chetu hivi karibuni kitasafiri kuelekea nchini Congo kwa ajili ya mchezo wetu huo, tunajua ugumu na umuhimu wa kupata matokeo katika mchezo huo lakini tumejipanga vizuri kupata matokeo chanya.

 

“Michezo mikubwa ya kirafiki ambayo tumecheza hivi karibuni kupitia Simba Super Cup imewaongezea wachezaji wangu hali ya kujiamini na ari ya kupambana kufanya vizuri hivyo nina imani kubwa tutafanya vizuri dhidi ya Vita.”

Stori: Said Ally na Joel Thomas, Dar

SIKU 100 za RAIS MWINYI, UCHUMI wa BLUE ZANZIBAR, AJIRA Kwa VIJANA | FRONT PAGE..

The post Mfaransa Simba SC Awapiga Biti Zito AS Vita appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand