-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

WACHEZAJI wa Yanga wameapa kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City utakaofanyika kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa Yanga katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo ambapo mchezo wa mzunguko wa kwanza baina ya timu hizo, Yanga ilishinda bao 1-0 mfungaji akiwa ni beki Lamine Moro.

 

Kiungo wa kati wa Yanga, Feisal Salum amesema malengo yao makubwa kuelekea mchezo huo ni kupata matokeo mazuri ambayo ni ushindi jambo ambalo wanaomba liweze kufanikiwa ili kupata ushindi.

 

“Kikubwa kuelekea mchezo huu ni kupata matokeo mazuri kwa timu ambayo ni ushindi, malengo yetu ni hayo sisi kama wachezaji tutapambania hilo ili liweze kufanikiwa, bila kusahau maombi ya mashabiki wetu ambayo ni muhimu kwetu,” alisema.

 

Naye beki wa kulia wa Yanga, Kibwana Shomari, alisema: “Msimu huu malengo yetu ni ubingwa, hivyo ni lazima tuweze kukusanya pointi nyingi ikiwemo katika mchezo wetu unaofuata wa ligi dhidi ya Mbeya City, tutapambana kufanikisha hilo.”

Stori: Marco Mzumbe,Dar es Salaam

The post Mastaa Yanga Wala Kiapo Kuiua Mbeya City appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand