-->

Type something and hit enter

On

Mwenyekiti wa kijiji cha Samanga Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Wilfredy Minja anadaiwa kumshambulia na bakora Asha Rajabu (28) ambae ni mjamzito na kumsababishia maumivu makali.


Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Ronald Makona amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo, amesema binti huyo alishambuliwa kwa bakora na mtuhumiwa huyo sehemu za makalio na mapajani na kumsababishia maumivu makali mwilini.


Kamanda Makona amesema kuwa Jitihada za kumtafuta na kumkamata mtuhumiwa zinafanyika na chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa, tayari timu yangu kwenda Marangu ili kujua ni kweli alikuwa na silaha hiyo.


Hata hivyo ujauzito wa Asha Rajabu, uliharibika kutokana na kipigo cha mwenyekiti huyo ambae pia inadaiwa alikuwa na bastola na kuifyatua juu, Asha yupo katika hospitali ya Kilema Wilayani Moshi akiendelea na matibabu.Click to comment
 
Blog Meets Brand