-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MABINGWA wa England klabu ya Liverpool, haitaruhusiwa kuingia nchini Ujerumani kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora dhidi ya RB Leipzig, kutokana na vizuizi vilivyowekwa na  Ujermani kwa wageni kutoka England ikiwa ni hatua za kujikinga na ugonjwa wa Covid-19.

 

 

Wizara ya mambo ya ndani ya Ujerumani imeiarifu klabu ya RB Leipzig kuwa mchezo dhidi ya Liverpool haujakidhi mahitaji kulingana na kanuni za sasa za kujikinga na virusi vya Corona.  Mchezo huo wa mkondo wa kwanza wa klabu bingwa ulaya hatua ya 16 bora umepangwa kuchezwa Februari 16, 2021.

 

 

Ujerumani imeweka vizuizi kwa baadhi ya wasafiri kuingia nchini humo kutoka kwenye mataifa ambayo yana maambukizi ya juu ya virusi vya Corona, ambapo England ni moja ya mataifa ambayo yapo kwenye orodha hiyo.

 

 

Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA) liliboresha kanuni zake juu ya janga la Corona, ambapo iliweka wazi kuwa kama timu mwenyeji haiwezi kuandaa mchezo kwenye uwanja wake basi inalazimika kutafuta uwanja mwingine ambao watautumia kuandaa michezo yao ya nyumbani, na kama watashindwa basi timu pinzani itapewa alama tatu na ushindi wa mabao 3-0.

 

Inaripotiwa kuwa uwanja wa Puskas uliopo mjini Budapest nchini Hungary ndiyo utakaotumika kuandaa mchezo huo kama uwanja wa nyumbani wa Leipzig lakini pia inatajwa mchezo huo unaweza kufanyika kwenye moja ya viwanja nchini England.

 

 

The post Liverpool Yapigwa Marufuku Kukanyaga Ujerumani appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand