-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

LICHA ya mshambuliaji mpya wa Yanga, Fiston Abdoulrazack kushindwa kufunga bao katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya African Sports kutoka Tanga, kocha mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amefunguka kuwa wachezaji wenzake walishindwa kumpa ushirikiano hususan kwenye pasi za mwisho ndiyo maana hakufunga.

 

 

Katika mchezo huo wa kirafiki uliofanyika Jumamosi katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar, Yanga ilifungwa kwa bao1-0 huku katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo Fiston na Wazir Junior wakianza.

 

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Kaze alisema amefurahishwa na uwezo aliouonyesha Fiston katika mchezo wake licha ya kushindwa kufunga bao kwani bado hajafanya mazoezi ya kutosha jambo ambalo linamfanya kushindwa kuwa fiti asilimia zote.

 

 

Kaze alisema kuwa, licha ya Fiston kujitahidi uwanjani wachezaji wenzake wanapaswa kufahamu namna ya kumtumia mchezaji huyo na namna ya kumtengea pasi za mwisho.

 

 

“Fiston amecheza vizuri licha ya kutofunga bao ukiamuangalia kwa jinsi alivyocheza utagundua kuwa hayupo fiti asilimia 100, hii ni kutokana na kufanya mazoezi kwa siku chache.

 

 

“Huu ni mchezo wake wa kwanza kwenye timu, amejitahidi. sina wasiwasi naye, ni mchezaji mzuri ambaye naamini ataongeza kitu katika kikosi chetu.

 

 

“Hajafahamiana vyema na wenzake uwanjani, wachezaji wenzake pia wanatakiwa kufahamu jinsi gani ya kumtumia Fiston, katika mchezo uliopita hakupewa pasi za kutosha kutoka kwa wenzake,”alisema Kaze.

 

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

The post Kaze Awavaa Mastaa Yanga appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand