-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

BIG bosi wa benchi la ufundi la Yanga, Mrundi Cedric Kaze ametamba kwamba hakuna namna ambayo itawafanya wapinzani wao Simba waweze kuwashusha katika uongozi wa Ligi Kuu Bara.

 

Kocha huyo ameongeza hilo linakuja kutokana na mikakati ya kuwa mabingwa ambayo wamejiwekea inayowafanya wapambane kwenye kila mechi yao.

 

Kocha huyo amefunguka hayo baada ya Yanga kutoka sare ya bao 1-1 na Mbeya City katika mechi ya ligi iliyopigwa juzi Jumamosi kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

 

Kwa sasa Yanga wapo kileleni kwa ligi wakiwa na pointi 45 zikiwa pointi sita mbele ya Simba wanaoshika nafasi ya pili na pointi 39.

 

Kaze ameliambia Championi Jumatatu, kwamba hawataruhusu kwa namna yoyote kikosi chao kushuka katika uongozi huo wa ligi hata itakapotokea wamepata matokeo mabaya.

 

“Tunajua kwamba wapinzani wetu wako nyuma yetu katika mbio hizi za ubingwa na matokeo yetu na Mbeya City wanaweza kuona kwao yana faida.

 

“Lakini tunajua wazi wanataka kutukwamisha lakini nia yetu inabaki palepale kuchukua ubingwa na tutapambana katika mechi zetu zijazo kuona hilo linafanikiwa,” aliweka nukta Mrundi huyo.

SAID ALLY, Dar es Salaam

The post Kaze Awatumia Ujumbe Mzito Simba SC appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand