-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

BAADA ya baadhi ya mashabiki kutoa lawama kuhusu kiungo mkabaji wa Yanga, Mukoko Tonombe kuanzia benchi katika mechi ya juzi dhidi ya Kagera Sugar, Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze ametaja sababu.Hiyo ikiwa ni dakika chache baada ya mchezo huo wa Ligi Kuu Bara kumalizika kwa sare ya mabao 3-3 dhidi ya Kagera Sugar uliopigwa juzi Jumatano kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Mukoko aliingia dakika ya 45 akichukua nafasi ya Zawadi Mauya na kutuliza sehemu ya kiungo huku akifunga bao la kuisawazishia timu hiyo.

“Hakuna kocha anayepanga timu ili apate matokeo mabaya ya kufungwa, hivyo leo (juzi) nilimpumzisha Tonombe kwa makusudi.“

 

Na hiyo ni kutokana na mfululizo wa michezo ya ligi ambayo ndani ya wiki moja tunatakiwa kucheza mechi tatu, hivyo kiafya ni hatari kwa wachezaji wangu.“

 

Hivyo, nikachukua maamuzi ya kumuweka benchi Tonombe na kumuanzisha Mauya, nimejifunza na nimeliona hilo nisingependa lawama ziende kwa wachezaji wangu, badala yake tunajipanga na michezo ijayo,” alisema Kaze

The post Kaze Afunguka Kumuweka Tonombe Bench appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand