-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Hitimana Thierry ameihofia timu ya Yanga kuelekea katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaopigwa leo kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar.

 

Mtibwa inashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Ihefu kwenye Uwanja wa Jamhuri.

 

Huku Yanga wakitoka sare ya mabao 3-3 dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Mkapa.Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Lamine Moro dakika ya 61.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Hitimana alisema kuwa: “Timu imefanya mazoezi ya mwisho leo (jana) kwenye uwanja tutakaocheza, wachezaji wote wapo fiti kuelekea katika mchezo huo.

 

“Tunatambua timu tunayocheza nayo ni kubwa lakini tutahakikisha tunapambana ili kupata ushindi katika mchezo huo,” alisema Hitimana.

STORI: LEEN ESSAU, Dar es Salaam

The post Hitimana Aihofia Yanga SC appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand