-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KATIKA kuelekea mchezo wao wa kwanza wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa Simba, Mfaransa, Didier Gomes, amewapa somo wachezaji wake nyota Luis Miquissone, Clatous Chama, Rally Bwalya na Meddie Kagere.

 

Hiyo ni baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC uliopigwa juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2.Timu hiyo Ijumaa hii inatarajiwa kucheza mchezo wake huo wa kwanza wa kimataifa wa Kundi A dhidi ya AS Vita ya DR Congo.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Gomes alisema kuwa viungo na washambuliaji wake wanatakiwa kufahamu nafasi za kufunga zinapatikana chache, hivyo wanatakiwa kuzitumia vema kwa kufunga mabao.

Gomes alisema kuwa hataki kuwaona tena wachezaji wake wakizichezea nafasi ambazo wanazipata ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika ligi na michuano ya kimataifa.Aliongeza kuwa, katika mchezo wa juzi dhidi ya Azam vijana wake walishindwa kuzitumia nafasi nne za wazi za kufunga mabao ambazo kama wangezitumia vema, basi matokeo yasingemalizika kwa sare hiyo.

 

“Katika mchezo wetu wa ligi dhidi ya Azam, timu ilicheza vizuri ikjiwemo kumiliki mpira na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga mabao, lakini umakini mdogo wa wachezaji wangu ukasababisha tupate sare ya mabao 2-2.“Kiukweli mchezo huu ingetakiwa tupate ushindi wa mabao manne, lakini umakini mdogo ukatugharimu.“

 

Hivi sasa tunaelekea kucheza kimataifa na kikubwa nimewataka vijana wangu waongeze umakini kwa kuhakikisha wanatumia vema kila nafasi watakayoipata.“

 

Tukiwa tunajiandaa na mchezo wetu dhidi ya AS Vita, nimewataka wachezaji wangu kutumia vema kwa kila nafasi tutakayoipata ya kufunga mabao kama kweli tunataka kutimiza malengo yetu ya kufuzu kucheza Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema Gomes

WILBERT MOLANDI

The post Gomes Ampa Mchongo Luis, Chama Simba SC appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand