-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

INGIZO jipya ndani ya kikosi cha Yanga, Fiston Abdoul Razack amesema kuwa atafunga bila kuogopa ndani ya Yanga kila atakapopata nafasi.

 

Nyota huyo leo anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi kitakachomenyana na Mbeya City na utakuwa mchezo wake wa kwanza baada ya kusaini dili la miezi sita ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze.

 

Raia huyo wa Burundi anaaminika kuwa mtatuzi wa ubutu wa safu ya ushambuliaji ya Yanga inayoongozwa na Michael Sarpong pamoja na Yacouba Songne ambao wote wamefunga mabao mannemanne.

 

Fiston amesema: “Ninajua wengi wanapenda kuniona ninafunga na kufanya kazi ya kuwapa ushindi ndani ya uwanja hilo linawezekana hivyo nitafunga bila kuogopa pale nitakapopata nafasi ya kucheza ndani ya uwanja.”

LUNYAMADZO MLYUKA,Dar es Salaam

The post Fiston: Yanga SC Tulieni, Nitafunga Tu appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand