Dozen Selection "Leo nimetafakari juu ya uwezo mkubwa alionao ROSA REE na uwezo mkubwa alionao kwenye muziki" - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Dozen Selection "Leo nimetafakari juu ya uwezo mkubwa alionao ROSA REE na uwezo mkubwa alionao kwenye muziki"


Kuna muda natamani Mungu angetupa macho matatu kwenye nyuso zetu, yaani Jicho moja lingekaa katikati ya uso pale juu kidogo na mstari unaotoka kwenye pua. Nawaza pengine jicho la tatu lingeweza kumsaidia Binadamu kuona na kutambua uwezo mkubwa alionao mwanadamu mwenzake na kumpongeza au ikibidi kumpa nguvu zaidi ya kufanikisha jambo lake.


Kwenye mpira waliona uwezo wa macho mawili ya Referee hayakutosha kuona bao la Frank Lampard ambalo alimtungua Manuel Neuer wa Ujerumani kwenye WC 2010, baada ya mpira kugonga mwamba na kuvuka mstari wa goli, mwamuzi alisema sio bao, Ndipo 2012 ikaasisiwa Goal Line Technology. Macho ya Referee ni mawili tu ndio maana pia ukaingizwa mfumo wa kumsaidia, maarufu VAR.


Bado naamini uwezo wa macho mawili hautoshi kuona mengi ya binadamu wenzetu hasa kwenye hii dunia ya kasi, japo nautukuza ukuu wa Mungu kwani nafahamu kuna ambao hawana macho kabisa, lakini naomba mnielewe kwa hili nitaloenda kuwaambia.


Leo nimetafakari juu ya uwezo mkubwa alionao ROSA REE, itakubidi uwe na jicho la TATU kuona kipaji na uwezo mkubwa alionao kwenye muziki. Kuna muda huwa namchukua halafu namdondosha pale Texas, naona Kabisa Thee Stallion akiweka mikono juu, hata Cardi B sidhani kama atakuwa na la kuongea juu yake. Tumebarikiwa kuwa na Female Rappers wachache TZ, @Rosa_Ree ni “Special” kuanzia kwenye staili yake ya kuchana na namna anavyobadilika kwenye kila wimbo wake, uwezo mkubwa wa kutumia Lugha zaidi ya moja unanipa ujasiri kwamba anafaa kuuzika kwenye soko la Kimataifa.


Mimi ni miongoni mwa wale ambao huvutiwa na mahojiano yake, upeo wake na kujieleza ni extraordinary, anajua anachokifanya na haitaji nguvu za KIUME kufika mbali bali nguvu yetu kwenye kusukuma kazi zake.


Kuna kipindi niliona akipambana kutafuta tobo kwa kuweka makazi nchini Kenya, niliona jinsi walivyompokea, nikajisemea moyoni kweli nabii hakubaliki kwao, ndio maana hata safari ya Samatta ilianzia Simba lakini Mazembe ndio walimpa nauli ya kufika Aston Villa!


Laiti tungekuwa na macho matatu pengine tungemfikisha mbali Rosa Ree, lakini macho yetu mawili yanaishia Ku-LIKE picha zake tu Instagram, na hata views zake YouTube pia hazina Nuru.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz