-->

Type something and hit enter

On 


DIRECTOR anayefanya poa kwa sasa kwenye tasnia ya burudani, Kennedy David Sanga ‘Director Kenny’ amesema kuwa anajisikia faraja kubwa kufanya kazi na msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’.

 

Akizungumza na Mikito Nusunusu, Kenny amesema kuwa tangu ameanza kufanya kazi na Diamond au Mondi, amekuwa na mafanikio makubwa kwenye maisha yake tofauti na hapo awali.

 

“Kwangu naona ni faraja kubwa kufanya kazi na Mondi kwa sababu ni mtu mkubwa na amefanya vitu vingi.

 

“Bongo na hata nje ya Bongo, nimepata vitu vingi kupitia yeye, maana kabla ya hapo nilikuwa sina hata uwezo kwa kijimudu kimaisha lakini kwa sasa hivi kila ninachotaka napata na pia kanifanya sasa hivi napata koneksheni za Kimataifa,” alisema Director Kenny.


STORI: KHADIJA BAKARI , RISASIClick to comment
 
Blog Meets Brand