-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

KOCHA Mkuu wa Simba, Mfaransa, Didier Gomes, ametamba kwamba sasa wako tayari kwa ajili ya kutafuta matokeo mazuri kwenye mechi zao za viporo ndani ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC na Dodoma Jiji.

 

Mfaransa huyo keshokutwa Alhamisi, kwa mara ya kwanza ataiongoza Simba katika Ligi Kuu Bara kwa kucheza dhidi ya Dodoma Jiji kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, kisha Jumapili ya wiki hii atakutana na Azam ndani ya Uwanja wa Mkapa, Dar.

Gomes ameliambia Spoti Xtra, kuwa licha ya kufahamu ugumu wa mechi hizo za ligi, lakini atakachokifanya ni kupambana kufanya vizuri ikiwa kwa sasa wapo kwenye kiwango kizuri baada ya kumaliza mechi za Simba Super Cup.

 

“Kitu kizuri ni kuwa tunaenda juu kila siku kwenye viwango vya uchezaji, tofauti na mechi ya kwanza tuliyocheza. Sasa tuko tayari kwa ajili ya mechi za kimataifa lakini hata kucheza mechi za ligi.“

 

Kwetu ligi kuu ndiyo tageti kwa ajili ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika na tunatakiwa kushinda mechi zetu dhidi ya Dodoma na Azam.

 

Ni mechi ngumu lakini tunatakiwa kuwa tayari kwa ajili ya kupambana na kufanya vizuri,” alimaliza Gomes.Wakati hayo yakitokea upande wa Simba, Azam wenyewe wanasema mchezo wao dhidi ya Simba hautakuwa rahisi kutokana na ubora wa wapinzani wao lakini kwa maandalizi ambayo wanaendelea kuyafanya wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri.

STORI: SAID ALLY NA HUSSEIN MSOLEKA, DAR

The post Didier Gomes Apata Mbinu za Kuwamaliza Dodoma, Azam appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand