-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

 

Mshambuliaji nyota wa klabu ya soka ya Juventus Cristiano Ronaldo, leo 5/2/2021 anatimiza miaka 36 tangu kuzaliwa kwake.

 

 

Ronaldo aliyezaliwa 5/2/1985 mji wa Madeira Ureno, amekuwa moja ya wachezaji wenye mafanikio makubwa sana katika historia ya mchezo wa soka Duniani, tangu alivyoanza rasmi soka la ushindani katika klabu ya Sporting CP ya nyumbani kwao mwaka 2003.

 

 

Alianza kufanikiwa kimataifa zaidi alivyojiunga na Manchester United mwaka huo huo 2003 na kudumu kwa miaka 6. Alifanikiwa kufanya makubwa, kwa kutwaa vikombe mbalimbali vya ligi za ndani pia kutwaa ubingwa wa ligi ya mabingwa Ulaya ‘UEFA’ mwaka 2008, pia alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Dunia ”Ballon d’or”.

 

 

Ronaldo alihamia klabu ya Real Madrid mwaka 2009 na kutambulisha ‘ufalme’ wake, kwa kufanya vizuri kama timu na yeye binafsi alifanikiwa zaidi kutwaa vikombe mbalimbali hasa kwenye ligi ya mabingwa wa Ulaya mara 4 katika uwepo wake Madrid kwa miaka takribani 10 ambapo ilikuwa mwaka 2013-14, 2015-16,2016-17 na 2017-18.

 

 

Mwaka 2018, Ronaldo alihamia klabu ya Juventus kwa uhamisho ulioshtua Dunia, wengi wakimtaja kuwa mzee na amekwisha kiuchezaji kutokana na umri wa miaka 33 aliyokuwa nayo , lakini huko nako alipata mafanikio ya kutosha ikiwemo ubingwa mara mbili mfululizo wa ligi ya Italy.

 

 

Cristiano Ronaldo anatimiza miaka 36 leo, umri ambao kisoka tunasema ni mzee lakini kwake imekuwa tofauti sana, kama uwezo unaongezeka kila kukicha, kwa sasa anaongoza kwa magoli katika ligi ya Italy akiwa amefunga magoli 15 katika mechi 16 akiwa amecheza jumla ya dakika 1,374 tu.

 

 

Ronaldo pia amefikia na kuvunja rekodi ya ya mfungaji bora wa muda wote wa magoli kwa mechi rasmi akiwa amefunga magoli 763 na kumpita Joseph Bican, mshambuliaji wa zamani wa Urusi aliyefunga magoli 762, amefanya haya akiwa anakaribia kutimiza miaka hiyo 36.

 

 

Takwimu za Ronaldo zinaonesha ameifungia Sporting CP magoli 5 katika michezo 31, Manchester United magoli 118 katika michezo 292, Real Madrid magoli 450 katika michezo 438 na Juventus magoli 87 katika michezo 112, pia ameweza kumudu kufunga magoli zaidi ya 300 akiwa amefikisha umri wa miaka 30.

The post Cristiano! Fundi wa Soka Anayezeeka na Utamu Wake appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand