-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) anayewakilisha Mkoa wa Dar es Salaam, Lameck Nyambaya amezitaka klabu zote zilizokuwepo katika mkoa wake kuhakikisha zinapambana zinabakisha taji la Ligi Kuu Bara jijini humo.

Timu za Dar es Salaam zinazoshiriki katika ligi hiyo ni nne ambazo ni Simba, Yanga, Azam FC pamoja na KMC FC.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Nyambaya ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar (DRFA), Nyambaya alisema kuwa kikubwa anataka kuona heshima ikiongezeka mkoani kwake.

 

Nyambaya alisema kuwa, ni faraja kwake kuona mkoa wake ukibeba taji mara tatu mfululizo ambalo lilikwenda Simba huku akizitaka timu hizo kupambana katika mzunguko huu wa ligi ubingwa huo ubakie tena kwa mara ya nne mfululizo.

“Ni faraja kwetu kama DRFA kuona timu zetu zinapata mechi kubwa za kirafi za kimataifa ambazo zitasaidia kwenye mashindano ya kimataifa na muendelezo wa ligi kuu katika raundi ya pili.

 

“Simba wamezialika Al Hilal na TP Mazembe, Azam FC wameomba mechi ya kirafiki dhidi ya TP Mazembe hiyo yote ni kuhakikisha ubingwa wa ligi unaendelea kubaki Dar.“

 

Ninaamini Yanga nao wapo katika maandalizi mazuri kuhakikisha wanafanikisha malengo yao kwa kucheza michezo ya kirafiki kujiandaa na mechi za mzunguko wa pili, hivyo niwatake mashabiki wa Dar, kujitokeza kwa wingi kuziunga mkono timu zao,” alisema Nyambaya.

The post Bosi TFF Azibana Simba,Yanga appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand