-->

Type something and hit enter

OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB

KATIKA Bundesliga Borussia Dortmund jana imelazimishwa sare ya 2-2 na Hoffenheim, shukrani kwa Erling Haaland aliyeisawazishia dakika ya 81 Uwanja wa Signal-Iduna-Park, hilo likiwa bao la 16 la msimu kwa Mnorway huyo aliyefunga wakati mchezaji mmoja wa wapinzani akiwa ameanguka chini baada ya kuumia.
Dortmund imeshinda mechi moja tu kati ya sita zilizopita za ligi na inajitoa tena kwenye Nne Bora katika mbio za kuwania tiketi ya Champions League na pengo linatarajiwa kuongezeka leo wakati Eintracht Frankfurt, Wolfsburg na Borussia Monchengladbach zikishuka dimbani.
Kocha wa Dortmund, Edin Terzic tayari amekalia kuti kavu baada ya kufungwa mechi tatu kati ya nne za Bundesliga na amezidi kujiweka pagumu kufuatia kumuweka benchi Nahodha, Marco Reus
 


Click to comment
 
Blog Meets Brand