-->

Type something and hit enter

OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB
MECHI mbili za viporo za Ligi Kuu ya Tanzania Bara zinachezwa leo, mabingwa watetezi, Simba SC wakimenyana na Azam FC kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam #AzamSports1HD na Namungo FC wakiwa wenyeji wa Ruvu Shooting kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi #AzamSports1HD.
Mara ya mwisho Azam FC kuifunga Simba SC ilikuwa ni Januari 28, mwaka 2017 waliposhinda 1-0, bao pekee la aliyekuwa Nahodha John Raphael Bocco dakika ya 70 akiupitia mpira ambao beki Mzimbabwe, Method Mwanjali alikuwa ‘anauchezea’ kwenye eneo la hatari na kwenda kumchambua kipa Mghana, Daniel Agyei.   
Siku hiyo vikosi vilikuwa; Simba SC; Daniel Agyei, Janvier Bokungu/Ibrahim Ajib dk59, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Abdi Banda, Method Mwanjali, Jonas Mkude, Said Ndemla, Jamal Mnyate/Shiza Kichuya dk47, Muzamil Yassin, Pastory Athanas na Juma Luizio/Laudit Mavugo dk65.
Azam FC; Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gardiel Michael, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Stephan Kingue/Mudathir Yahya dk77, Himid Mao, Joseph Mahundi, Frank Domayo, John Bocco/Abdallah Kheri dk83 na Ramadhani Singano ‘Messi’/Yahya Mohammed dk63.
Kwa ujumla, katika mechi 24 za Ligi Kuu ambazo timu hizo zimekutana hadi sasa, Simba SC wameshinda 11, Azam FC wameshinda sita na nyingine sita wametoka sare.


REKODI YA SIMBA NA AZAM FC LIGI KUU:
P W D L Pts
Azam FC 24 6 6 11 24
Simba SC 24 11 6 6 39
MATOKEO YA MECHI ZILIZOPITA AZAM V SIMBA
Machi 4, 2020: Azam FC 2-3 Simba SC
Oktoba 23, 2019: Simba SC 1-0 Azam FC
Mei 13, 2019: Simba SC 0-0 Azam FC
Februari 22, 2019: Azam FC 1-3 Simba SC
Februari 7, 2018: Simba 1-0 Azam FC
Septemba  9, 2017: Azam FC 0-0 Simba SC (Chamazi)
Januari 28, 2017: Simba SC 0-1 Azam FC
Septemba 17, 2016: Azam FC 0-1 Simba SC
Mei 1, 2016: Simba SC 0-3 Azam (Dar)  
Desemba 12, 2015: Azam FC 2-2 Simba SC   
Januari 25, 2015: Azam FC 1-1 Simba SC  
Mai 3, 2014: Simba SC 2-1 Azam FC 
Machi 30, 2014: Azam FC 2-1 Simba  
Oktoba 28, 2013: Simba SC 1-2 Azam FC  
Aprili 14, 2013: Azam FC 2-2 Simba SC   
Oktoba 27, 2012: Simba SC 3-1 Azam FC   
Februari 11, 2012: Simba SC 2-0 Azam FC
Septemba 11, 2011: Azam FC 0-0 Simba SC
Januari 23, 2011: Simba SC 2-3 Azam FC
Septemba 11, 2010: Azam FC 1-2 Simba SC
Machi 14, 2010: Azam FC 0-2 Simba SC  
Oktoba 24, 2009: Simba SC 1-0 Azam FC  
Machi 30, 2009: Azam FC 0-3 Simba SC
Okt 4, 2008: Simba FC 0-2 Azam FC


Click to comment
 
Blog Meets Brand