Albamu ya Darasa yafanya vizuri, yafikisha watazamaji milioni 138 - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Albamu ya Darasa yafanya vizuri, yafikisha watazamaji milioni 138

 Album ya rapa Darassa  a.k.a Mr Burudani, "Slave Becomes A King", inaendelea kufanya vizuri duniani, ikiwa tayari ina miezi miwili pekee tangu iachiwe rasmi. Iliachiwa mwishoni mwa mwaka, na tayari imefikisha jumla ya streams MILIONI 138 kwenye majukwaa yote ya kusikiliza na kupakua muziki duniani (Digital Platforms).

"Slave Becomes A King" ina jumla ya nyimbo 21 alizowashirikisha wasanii tofauti tofauti kama #Alikiba, Marioo, Nandy, BillNass, ShoMadjozi na wengine wengi. Pia hii ndio album yake ya kwanza kwenye muziki wake.

 DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL HAPA KUPATA HIZI HABARI KWENYE SIMU YAKO HATA BILA BUNDLE

Sanjali na hilo, Mr Burudani Darassa tayari kashaachia video mbili toka kwenye album hiyo, video hizo ni pamoja na Proud Of You (ft. AliKiba & Waiter) ukiacha 'I Like It' (ft. Sho Madjozi) ambayo ilitangulia mwaka jana.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz