-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

YANGA imetinga nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Namungo FC bao 1-0, mchezo uliochezwa jana Januari 8, 2020 kwenye Uwanja wa Amaan kisiwani hapa.

Bao la Yanga lilifungwa na Zawadi Mauya dakika ya 24 baada ya kuliga shuti lililotinga moja kwa moja golini katika mechi iliyokuwa na ushindani mkubwa.

Mechi ya kwanza Yanga walichez ana Jamhuri ya kisiwani Pemba ambapo timu hizo zilitoka sare tasa hivyo mechi ya leo kwa Yanga itatoa mwanga ya wao kusonga mbele kama matokeo yatabaki hivi hivi.

Kwa upande wa Namungo wao ni mechi ya kwanza ambapo baada ya hii watacheza na Jamhuri ili kujua hatma yao kwenye mashindano haya ambayo kilele chake ni Januari 13 mwaka huu.

Timu zote mbili kipindi cha kwanza zilicheza kwa kushambuliana na kukosa nafasi kadhaa za wazi ambapo Namungo dakika ya 33 walikosa mpira ukiwa ni wa piga nikupige langoni mwa wapinzani nao.

The post Yanga Yatangulia Nusu Fainali Mapinduzi appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand