-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

TIMU ya Yanga Princess inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara, imeen-delea kuwa moto wa kuotea mbali katika ligi hiyo baada ya kuichapa Alliance Queens ma-bao 5-0 katika mchezo uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini hapa.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa tangu kipindi cha kwanza, timu zote zilionekana kushambuliana kwa zamu, lakini kipindi cha pili, Alliance walipotea na kuruhusu kipigo hicho kutoka kwa Yanga Princess ambayo imemaliza mzunguko wa kwanza bila kupoteza mchezo wowote.Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha wa Alliance Queens, Ezekiel Chobanka, amesema:

“Tumepoteza mchezo dhidi ya Yanga Princess kwa kuwa wenzetu walikuwa vizuri kuliko sisi, ukiangalia safu yao ya ushambuliaji ipo vizuri kuliko yetu, yaani wana washambuliaji wanaoweza kufunga wakati wowote.”

 

Naye Kocha wa Yanga Princess, Edna Lema, ameliambia Spoti Xtra kwamba: “Malengo yetu ni kutwaa ubingwa, tumeamua kuhakikisha kila mchezo tunashinda na najua kwamba tunapofanya vizuri kila mchezo tunaweza kufikia malengo hayo. Pia tunataka kuweka rekodi ya kumaliza ligi bila kufungwa.”

 

Yanga Princess ambao ni vinara wa ligi hiyo, wamemaliza mzunguko wa kwanza kwa kucheza mechi 11, wameshinda kumi na sare moja, huku wakikusanya pointi 31.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

The post Yanga Princess Haikamatiki WPL appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand