-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa maendeleo ya nyota wao watatu ambao ni majeruhi ndani ya kikosi hicho ambao ni Said Ntibanzokiza, Yacouba Songne na Dickson Job yanaleta matumaini hivyo mashabiki wasiwe na presha.

 

Said au Saido ambaye ni kiungo mshambuliaji aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons huku Yacouba alipata maumivu kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Azam FC na Job yeye alipata maumivu ya paja akiwa kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh alisema kuwa kwa sasa wachezaji wanaendelea na mazoezi huku wale wanaosumbuliwa na majeraha wakiwa na maendeleo mazuri.

 

“Kuhusu Job huyu tayari ameanza mazoezi mepesi na wachezaji wenzake ambao wapo kambini hivyo tupo imara na nina amini kwamba mpaka ligi itakaporudi kila kitu kitakuwa sawa.“Yacouba na Saido nao pia bado hawajawa fiti ila nao maendeleo yao ni mazuri hivyo mashabiki wasiwe na mashaka kuhusu wachezaji hawa,” alisema Saleh

The post Yacouba, Saido Washusha Presha Yanga appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand