-->

Type something and hit enter

On 


Kuelekea mchezo wa Simba Super Cup leo Januari 31, 2021 kati ya TP Mazembe dhidi ya Simba SC kwenye uwanja wa Mkapa, hawa ndio wachezaji wa Simba SC ambao hawatakuwa sehemu ya mchezo huo.

 

Kwa mujibu wa meneja wa timu ya Simba SC Abbas Ally, wachezaji wa timu hiyo ambao walikuwa na timu ya taifa kwenye michuano ya CHAN kama Aishi Manula hawatacheza licha ya kujiunga na kambi ya Simba SC.

Wengine ni Shomari Kapombe, Said Ndemla, Ibrahim Ame na John Bocco, ambao nao watakosa mchezo wa leo dhidi ya TP Mazembe. 

 

Mchezo huo pia utatangazwa mubashara kupitia East Africa Radio na watangazaji Mtaalam wa Soka Ibra Kasuga na Abissay Stephen kuanzia saa 9:30 mchana ambapo studio watakuwepo David Kampista na Tigana Lukinja.Click to comment
 
Blog Meets Brand