-->

Type something and hit enter

By OnPakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako na Kuasoma habari zote hata kama hauna MB

WAKATI Yanga ikiwa inaongoza ligi, kocha mkuu wa timu hiyo, Mrundi, Cedric Kaze amekuwa akitumia kiasi cha shilingi milioni nane kwa siku 30 kulipa kodi katika nyumba anayoishi na familia yake.

 

Kaze amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Canada katika Akademi ya Barcelona ambapo ameiwezesha timu hiyo mpaka sasa kuchukua ubingwa wa Kombe la Mapinduzi huku wakiongoza Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 44 wakifuatiwa na Simba wenye pointi 35.

 

Kaze anayekunja mshahara wa dola 10,000 (Sh mil 23), analipiwa dola 120 (Sh 277,801) kwa ajili ya kulala tu.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga, kimeliambia Championi Jumamosi kuwa, kocha huyo yeye ameamua kuishi kwenye apartment akiwa na familia yake ambapo kwa siku analipia dola 120 kwa ajili ya kulala pekee pale Palm Village Mikocheni jijini Dar karibu na mabosi wa Azam FC.

 

“Mwalimu yeye anaishi katika apartment ya Palm Village kwa sababu yupo na familia yake hapa nchini, kwa upande wa bei yake pale imechangamka kidogo.“

 

Pale halipii yeye bali uongozi ndiyo unalipia, kwa siku moja wanasema ni dola 120 ingawa tofauti huwa wanalipa kwa bili ya mwezi ambayo inafika milioni nane kwa kuwa familia yake bado inaishi pale licha ya mwalimu mwenyewe muda mwingi kuwa Avic Town inapokuwa timu wakati wote,” alisema mtoa taarifa.

Stori: Ibrahim Mussa na Mussa Mateja

The post Usingizi wa Kaze Yanga ni Milioni Nane appeared first on Global Publishers.Click to comment
 
Blog Meets Brand