Unaambowa Esma Platnumz Yamkuta Ya Qeen Darleen..Nyumba za Kifahari Zawaponza - EDUSPORTSTZ

Latest

Unaambowa Esma Platnumz Yamkuta Ya Qeen Darleen..Nyumba za Kifahari Zawaponza

 Esma Yamkuta Ya Darleen

January 9, 2021 by Global Publishers
WASWAHILI wanasema kuimba ni kupokezana! Baada ya hivi karibuni msanii wa Bongo Fleva na memba wa Lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Mwanahawa Abdul ‘Queen Darleen’, kuutema mjengo wa kifahari aliokuwa akiishi na mumewe maeneo ya Mbezi Beach, Dar es Salaam na kurudisha majeshi nyumbani kwao Sinza, imeripotiwa kuwa ndugu yake Esma Khan naye yamemkuta yaleyale.


 


Habari kutoka chanzo chetu zinaeleza kuwa Esma amelazimika kuhama kwenye jengo la kifahari la ghorofa alilokuwa akiishi maeneo ya Mikocheni akiwa na mtalaka wake Yahya Msizwa.


 


Msizwa na Esma waliachana hivi karibuni ambapo inadaiwa ndiyo sababu iliyomfanya Esma ambaye ni dada wa msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’ kuondoka kwenye nyumba hiyo ambayo kwa sasa inatafutiwa wateja na madalali.


 


Kufuatia hatua hiyo hali kwenye mitandao ya kijamii ilitibuka baada ya kile kinachotajwa kuwa Esma alifurahia ‘anguko’ la nduguye Queen Darleen ‘kurudisha mpira kwa kipa’ jambo ambalo wanaomkebehi wanasema naye yamemkuta.


 “Wakati mwenzake anarudi nyumbani kwao yeye alifurahi sasa zamu yake kuonja machungu maisha ya kutambia wanaume siku hizi hayana mpango,” aliandika mtu mmoja kwenye mtandao wa kijamii kuonesha hisia hasi kwa kitendo cha Esma kuihama nyumba hiyo ya thamani.

 

Hata hivyo, habari zilizopatikana kutoka vyanzo vyetu ni kwamba Esma kwa sasa anaishi Mbezi Beach, Dar akiwa na mzazi mwenzake Hamad Manungwi ‘Petit Man’ ambaye pia alikuwa mumewe kabla hajaachana naye na kuolewa na Msizwa ambaye naye wamebwagana.

 

Inaelezwa kuwa baada ya ndoa ya Esma na Msizwa kuvunjika dada huyo wa Diamond aliona isiwe shida kwani hakutupa cha zamani alipokipata kipya na hivyo kurejea kwa mumewe wa zamani, Petit Man.

 

Taarifa za chini ya kapeti zilisema kuwa sababu ya Queen Darleen kuuhama mjengo wa kifahari aliokuwa akiishi ni kushindwa kulipa kodi, lakini kwa Esma hali imekuwa kimya, ingawa ukweli ni kwamba tayari ameondoka kwenye nyumba hiyo ya ghorofa.

 

Mwandishi wetu alipomtafuta Queen Darleen kutaka ukweli kuhusu madai ya kushindwa kulipa kodi aliwaka na kuongeza kuwa:


“Kama nimerudi nyumbani kuna tatizo gani, uzuri sijaenda kwa mtu, nimerudi kwetu.”


Esma alipotafutwa mara kadhaa kwa njia ya simu hakupatikana na alipotumiwa ujumbe kwa njia ya WhatsApp alionekana kuusoma lakini hakuujibu.Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.