Ukweli Lulu Kumburuza Wema Mahakamani - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Ukweli Lulu Kumburuza Wema Mahakamani
HALI ya hewa imechafu! Siku chache baada ya Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu kuibua mauaji ya aliyekuwa mwigizaji nguli wa filamu nchini Tanzania, Marehemu Steven Kanumba kupitia kipindi chake cha Cook With Wema Sepetu, mambo mjini yamekorogeka.

 

Baadhi ya watu wamekuwa wakishinikiza miss huyo ambaye pia ni msanii wa filamu za Kibongo ashtakiwe na kuruzwa mahakamani kwa kile kinachotajwa kumwalika mama mzazi wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa ambaye alitumia kipindi hicho kutonesha machungu ya mwingizaji Elizabeth Michael, ‘Lulu’ aliyekutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia Kanumba, Aprili 7, 2012 na kutupwa jela miaka mwili.

 

SHINIKIZO LA WEMA KUSHTAKIWA

“Ni mahojiano ya ovyo, yanayoweza kuibua hisia mbaya kwa jamii kuhusu Lulu, mimi namshauri amchukulie hatua za kisheria.”“Mtu alishahukumiwa, akafungwa, katoka jela, lakini bado unatumia kipindi chako kumhoji mama mzazi kuhusu kifo cha mwanaye, hii siyo sawa, ningekuwa Lulu ningempeleka Wema mahakamani…”“Huu ni uchochezi wa wazi na sheria iko wazi, Lulu amfikishe Wema mahakamani kwa uchochezi.”Hizi ni baadhi ya komenti mitandaoni ambazo zilikuwa zinamshawishi Lulu kumchukulia Wema hatua za kisheria.Mbali na komenti za aina hiyo, jicho letu mitandaoni limebaini kuwepo kwa vita kubwa kati ya timu Wema (Team Wema) na ile ya Lulu (Team Lulu) na kwamba malumbano ya maneno kuhusu ishu hiyo yamefika mahali pa kutoleana maneno machafu ya nakuudhi.

 

HUU HAPA UKWELI WA WEMA KUWEZA KUSHTAKIWA

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, Wakili wa Kujitegemea, Albert Msando anasema kuwa, suala la Lulu kumpeleka Wema Polisi au mahakamani haliwezekani kwa sababu jamii ipo huru kujadili tukio hilo la marehemu Kanumba.

 

Alisema licha ya kwamba Lulu tayari alishtakiwa, akahukumiwa adhabu ya kuua bila kukusudia na kwa kuwa sasa yupo huru, hawezi kuizua jamii kujadili suala hilo.

 

“Ila sasa hapo inategemea jamii inalijadili kwa mrengo gani, kama jamii inajadili kwa namna ya kutaka kulipiza kisasi, kwamba kuna mtu amejitokeza kumtishia maisha au kumtendea jambo lolote baya…hapo atakuwa amekwenda kinyume cha sheria na Lulu atalazimika kumshtaki mtu huyo,” anasema Msando.

 

Anasema kuwa, kwa upande wa Mama Kanumba kuendelea kusisitiza kuwa hatamsamehe Lulu katika tukio la mauaji ya mwanaye, hilo ni suala ambalo ameamua kulibeba mwenyewe.“Kwa sababu hata vitabu vya dini vimeandika, kutosamehe ni sawa na kujibebesha mzigo mwenyewe.

 

Kwa hiyo hapo Lulu hana shida na Mama Kanumba, bali Mama Kanumba ndiye mwenye shida kwa kujibebesha mzigo wa kutosamehe,” anasema.Msando aliongeza kuwa, haoni haja ya jamii kuendelea kulipa uzito suala hilo la marehemu Kanumba kwa kuwa linaweza kumsababishia Lulu kupatwa na msongo wa mawazo kisha kuchukua uamuzi mbaya.

 

LULU ANASEMAJE KUHUSU HILI

Wakati mjadala wa mama Kanumba kufunguka laivu kwenye kipindi cha Wema kuwa angali ana kinyongo na Lulu mwenyewe aliandika kupitia ukurasa wake wa Instagram:“Tupo busy na kujenga

 

nyumba, wengine wapo busy na kujenga majungu.Tunawapa mitano tenaaaa. Huu mwaka mtajibebaaa mbona ndiyo kwanza mwezi wa kwanza siku ya 9 leo. Bado sanaaa.”

 

Baada ya kuandika hivyo, baadhi ya watu walimfuata na kutupia komenti zao zenye maudhui tofauti, nyingine za kumponda na nyingine za kumtia moyo kama hii;“Achana na wale wazee wote wameshajichokea kama Wema anapambana na upepo usimdondoshe.”Hata hivyo, wachunguzi wa mambo wanasema tayari Lulu amesitisha urafiki wake na Wema kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa maana ya kum-unfollow mazima.

 

WEMA ANASEMAJE?

Chanzo cha karibu na msanii huyo mwenye mashabiki lukuki kinasema kuwa baadhi ya watu wake wa karibu walimsihi Wema amuombe msamaha Lulu yaishe ili kujenga umoja na upendo kati yao.Hata hivyo, inadaiwa kuwa Wema amegoma kumuomba msamaha Lulu kwa kile alichosema; “Hakuna mahali popote nilipomkosea sasa nimuombe masamaha wa nini?”

 

MSAMAHA NA KINYONGO CHA MAMA KANUMBA

Rekodi za sarakasi za Mama Kanumba na Lulu zinaonesha kuwa amekuwa na desturi ya kumsamehe msanii huyo na baadaye kurejea kwenye kinyongo chake.Aprili 9, 2013 katika sala maalum ya kumuombea mwanaye kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar alikozikwa; Mama Kanumba alitamka wazi kuwa amemsamehe Lulu na kwamba yote yaliyotokea amemwachia Mungu.Kwa msingi huo kitendo cha juzi kutamka kuwa angali ana kinyongo naye ni jambo linaloonesha kuwa amekuwa na tabia ya kusamehe bila kusahau.

GPL


Je wajua!!!???

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click 👉👉👇👇👇https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.

No comments:

Post a Comment

Je Wajua??

Kiwangadoctors ni madaktari ambao wanasifika East Africa na Africa kwa ujumla,Kiwangadoctors wanatatua shida mbalimbali za maisha kama,kurudisha mpenzi,kupandishwa cheo,kupata kazi,kupata mimba kwa wale waliokosa,Nguvu za kiume na kushinda michezo ya Batinasibu pia kiwanga Doctors wanatibu mgonjwa sugu kama,Sukari ,Pressure pamoja na stroke.
Wasiliana na kiwanga Doctors kwa number/WhatsApp +254769404965 Au kwa barua pepe kiwangadoctors@gmail.com. taarifa zaidi click >>>>https://www.kiwangadoctors.com kwa taarifa zaidi.
Edusportstz